Pages

Monday, June 30, 2014

MISS SHINYANGA 2014 APATIKANA,TAZAMA PICHA KIBAO HAPA



Hatimaye mkoa wa Shinyanga umepata mrembo(Redd's Miss Shinyanga 2014),mrembo huyu si mwingine bali ni  Nicole Franklyn Sarakikya(katikati) aliyekuwa akiwakilisha wilaya ya Kishapu,lakini pia Miss Kishapu 2014.Mashindano ya kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga yamefanyika Juni 28,2014 mjini Kahama katika ukumbi wa NSSF yakiwa yameandaliwa na Asela Promotion ikisimamiwa na bi Asela Magaka.Waliosimama ni warembo ambao waliingia katika top 5.

Washiriki  walioingia 5 bora katika  shindano la Redd's Miss Shinyanga 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Kahama ambapo jumla ya warembo 20 kutoka maeneo mbalimbali kutoka mkoa wa Shinyanga walikuwa wakiwania taji hilo.Kati ya hao 5 bora mmoja aliibuka mshindi wa kwanza
Mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho ni bi Nicole Franklyn Sarakikya kutoka wilaya ya Kishapu,mshindi wa pili ni Mary Emmanuel kutoka Ushetu,mshindi wa tatu ni Rachel Judica kutoka Shinyanga vijijini ,mshindi wa nne ni  Nyangi Warioba kutoka Msalala,  na mshindi wa 5 Neema Kakimpa kutoka wilaya ya Kahama
Mshindi wa taji la Redd's Miss Shinyanga 2014 bi Nicole Franklyn Sarakikya kutoka wilaya ya Kishapu.Katika mashindano hayo ya kupata mrembo wa mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Asela Promotions,mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha Shilingi la 500,000/= na Laptop moja,mshindi wa pili shilingi 350,000/= mshindi wa tatu shilingi 250,000/=,mshindi wa 4 shilingi 150,000/= na mshindi wa tano shilingi 150,000/= huku washiriki wengine waliosalia kati ya 20 wakipata shilingi 100,000/= kila mmoja.
Katikati ni mshindi wa kwanza shindano la Redd's Miss Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya,kushoto ni mshindi wa pili ni Mary Emmanuel,kulia ni mshindi namba tatu  ni Rachel Judica ambao watashiriki katika shindano la kutafuta mrembo wa kanda ya ziwa lililoandaliwa na Flora Salon

Saturday, June 21, 2014

AMANI WA KENYA NA MO MUSIC KUKAMUA MISS SHINYANGA 2014‏




Warembo hao wakifanya mazoezi katika ukumbi wa Ihesa Hotel & Resort Ltd ya mjini Kahama.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mo Music akiwa katika pozi siku ya jana Global Tv Online.
Mwanamuziki, Amani wa Kenya.
Na Mwandishi Wetu (Ali Lityawi),
Kahama,
Juni 15, 2014
WAREMBO 20 wanatarajia kupanda jukwaani Juni 28, mwaka huu ndani ya ukumbi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii ( NSSF) wilayani Kahama kuwania Taji la Redd's Miss Shinyanga 2014.

Kwa mujibu wa waratibu, Kampuni ya Asela Promotion, shindano hilo litashirikisha Warembo kutoka katika Wilaya sita za Mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Kahama, Shinyanga Mjini, Msalala Shinyanga Vijijini na Ushetu.
Mratibu wa shindano hilo, Asela Magaka alisema mwaka huu anatarajia Redd's Miss Tanzania 2014 atatoka mkoa wa Shinyanga kutokana na warembo waliopo kambini kuwa na vigezo, mvuto mkubwa na viwango vinavyofaa kunyakua taji hilo.
Magaka aliwataja warembo hao kuwa ni Aisha Ally, Grace Lyimo, Pendo Maxmillian, Mary Bugingo, Irine Hamedi, Neema Kakimpa,Jacquline Robert, Nilam Siraji, Grace Kimaro, Sophia Mhina, Jacline Kimambo, Rose Shunda na Lawrancea Mathew.
Aliwataja Warembo wengine kuwa ni Rachel Mushi, Hadija Nyanda, Nyangi Warioba, Rockie Bangili,Jacline Jacksoni, Lukia Samili na Nicole Sarakikya hivyo kuwataka mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa taji la Mrembo wa Mkoa wa Shinyanga.
“Warembo tayari wameanza mazoezi katika ukumbi wa Ihesa Hotel & Resort Ltd ya mjini Kahama na washindi watatu watawakilisha mkoa wa Shinyanga katika michuano ya Kanda” Alisema Asela Magaka.
Aidha aliwataja wadhamini wa Shindano hilo kuwa ni SSCN TV ya Mjini Kahama, Nonema Investiment, Trixie Social Media Market, Nyamizi Secretarial Service, Royal Supermarket, NSSF, Coca Cola, Redd's na Global Publishers.
Wengine ni pamoja na Clouds FM, Three Jays’s Inverstment, CXC Africa, Williamson Diamond, Saluti5, Ihesa Hotel, Kahama Commonity Health Dispensary, Tulliz Fashion, Ngeleja Gold Mine, Kahama Motel, Charitk Pub, Glory Pads na Barrick Buzwagi.