Pages

Monday, June 30, 2014

MISS SHINYANGA 2014 APATIKANA,TAZAMA PICHA KIBAO HAPA



Hatimaye mkoa wa Shinyanga umepata mrembo(Redd's Miss Shinyanga 2014),mrembo huyu si mwingine bali ni  Nicole Franklyn Sarakikya(katikati) aliyekuwa akiwakilisha wilaya ya Kishapu,lakini pia Miss Kishapu 2014.Mashindano ya kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga yamefanyika Juni 28,2014 mjini Kahama katika ukumbi wa NSSF yakiwa yameandaliwa na Asela Promotion ikisimamiwa na bi Asela Magaka.Waliosimama ni warembo ambao waliingia katika top 5.

Washiriki  walioingia 5 bora katika  shindano la Redd's Miss Shinyanga 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Kahama ambapo jumla ya warembo 20 kutoka maeneo mbalimbali kutoka mkoa wa Shinyanga walikuwa wakiwania taji hilo.Kati ya hao 5 bora mmoja aliibuka mshindi wa kwanza
Mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho ni bi Nicole Franklyn Sarakikya kutoka wilaya ya Kishapu,mshindi wa pili ni Mary Emmanuel kutoka Ushetu,mshindi wa tatu ni Rachel Judica kutoka Shinyanga vijijini ,mshindi wa nne ni  Nyangi Warioba kutoka Msalala,  na mshindi wa 5 Neema Kakimpa kutoka wilaya ya Kahama
Mshindi wa taji la Redd's Miss Shinyanga 2014 bi Nicole Franklyn Sarakikya kutoka wilaya ya Kishapu.Katika mashindano hayo ya kupata mrembo wa mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Asela Promotions,mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha Shilingi la 500,000/= na Laptop moja,mshindi wa pili shilingi 350,000/= mshindi wa tatu shilingi 250,000/=,mshindi wa 4 shilingi 150,000/= na mshindi wa tano shilingi 150,000/= huku washiriki wengine waliosalia kati ya 20 wakipata shilingi 100,000/= kila mmoja.
Katikati ni mshindi wa kwanza shindano la Redd's Miss Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya,kushoto ni mshindi wa pili ni Mary Emmanuel,kulia ni mshindi namba tatu  ni Rachel Judica ambao watashiriki katika shindano la kutafuta mrembo wa kanda ya ziwa lililoandaliwa na Flora Salon

Miss Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya

Msanii Mo Music akifanya yake jukwaani
Kabla ya washindi kutangazwa majaji wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kinajiri katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama.Katikati ni chief judge Flora Lauo kutoka Mwanza,kushoto ni  bi Aneth Dotto kutoka Arusha Miss Shinyanga  mwaka 2003,kulia ni jaji Lutufyo Kanyenye
Kulia ni bi Asela Magaka ambaye ni mkurugenzi wa Asela Promotions waandaaji wa mashindano ya Miss Shinyanga 2014,wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya,wa tatu ni naibu waziri wa kilimo,chakula na ushirika Godfrey Zambi wakifuatilia shindano la Miss Shinyanga 2014.
Waandishi wa habari kutoka Kahama fm hawakuwa nyuma kushuhudia nani ataibuka mshindi katika shindano la mrembo wa mkoa wa Shinyanga
Washiriki 20 wa shindano la Miss Shinyanga 2014 wakitoa show ya ufunguzi

Burudani kutoka kwa mwimbaji wa taarabu nchini Mzee Yusuph ikiendelea,wakazi wa Kahama na wananchi mbalimbali kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga walipandwa na mzuka na kuamua kucheza
 Mshiriki wa Shindano la kutafuta mrembo mwenye kipaji (Miss Talent Shinyanga 2014) lililofanyika mjini Shinyanga Juni 25,2014 katika ukumbi wa NSSF,Irene Makwaiya kutoka wilaya ya Kishapu akionesha kipaji chake cha kuimba katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama
Kazi haikuishia kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga.Jukwaani ni Asela Magaka ambaye ni mkurugenzi wa Asela Promotions waandaaji wa mashindano ya Miss Shinyanga 2014 akimtangaza mshindi wa Shindano la kutafuta mrembo mwenye kipaji(Miss Talent Shinyanga 2014) lililofanyika mjini Shinyanga Juni 25,2014 katika ukumbi wa NSSF ambapo warembo 5 bora walipatikana na jana mshindi alitangazwa ambaye ni Irene Makwaia kutoka Kishapu


Miss Talent Shinyanga 2014 Irene Makwaiya kutoka wilaya ya Kishapu aliyeibuka na kitita cha shilingi 300,000/=

 Kushoto ni msanii Amani kutoka Kenya akifuatilia kilichokuwa kinajiri,baadaye akafanya show baaabu kubwaa katika shindano kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga 2014
Baada ya shindano la Miss Shinyanga kuisha-kulia ni Ice Joseph kutoka Lewis Intertainment katika picha ya pamoja na mshindi wa pili bi Mary Emmanuel(kushoto)-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment