Kahama,
Juni 15, 2014
WAREMBO 20 wanatarajia kupanda jukwaani Juni 28, mwaka huu ndani ya ukumbi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii ( NSSF) wilayani Kahama kuwania Taji la Redd's Miss Shinyanga 2014.
Kwa mujibu wa waratibu, Kampuni ya Asela Promotion, shindano hilo litashirikisha Warembo kutoka katika Wilaya sita za Mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Kahama, Shinyanga Mjini, Msalala Shinyanga Vijijini na Ushetu.
Mratibu wa shindano hilo, Asela Magaka alisema mwaka huu anatarajia Redd's Miss Tanzania 2014 atatoka mkoa wa Shinyanga kutokana na warembo waliopo kambini kuwa na vigezo, mvuto mkubwa na viwango vinavyofaa kunyakua taji hilo.
Magaka aliwataja warembo hao kuwa ni Aisha Ally, Grace Lyimo, Pendo Maxmillian, Mary Bugingo, Irine Hamedi, Neema Kakimpa,Jacquline Robert, Nilam Siraji, Grace Kimaro, Sophia Mhina, Jacline Kimambo, Rose Shunda na Lawrancea Mathew.
Aliwataja Warembo wengine kuwa ni Rachel Mushi, Hadija Nyanda, Nyangi Warioba, Rockie Bangili,Jacline Jacksoni, Lukia Samili na Nicole Sarakikya hivyo kuwataka mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa taji la Mrembo wa Mkoa wa Shinyanga.
“Warembo tayari wameanza mazoezi katika ukumbi wa Ihesa Hotel & Resort Ltd ya mjini Kahama na washindi watatu watawakilisha mkoa wa Shinyanga katika michuano ya Kanda” Alisema Asela Magaka.
Aidha aliwataja wadhamini wa Shindano hilo kuwa ni SSCN TV ya Mjini Kahama, Nonema Investiment, Trixie Social Media Market, Nyamizi Secretarial Service, Royal Supermarket, NSSF, Coca Cola, Redd's na Global Publishers.
Wengine ni pamoja na Clouds FM, Three Jays’s Inverstment, CXC Africa, Williamson Diamond, Saluti5, Ihesa Hotel, Kahama Commonity Health Dispensary, Tulliz Fashion, Ngeleja Gold Mine, Kahama Motel, Charitk Pub, Glory Pads na Barrick Buzwagi.
No comments:
Post a Comment