

Anajiita Mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha
mashabiki wake kwa shangwe huku mayowe yakitawala kila kona ya uwanja wa
Kambarage usiku huu ndani wakati tamasha la Serengeti fiesta
likiendelea kurindima usiku huu.

Mtoto wa Mama Saidi a.k.a Cheke akiimba kwa hisi jukwaani.

Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoko akiimba jukwaani usiku huu sambamba na madensa wake (hawapo pichani).

Tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu.

Mashabiki wake wanamuita Kinga Zilla kutoka Sala Sala,lakini pia jina
la Godzilla limemuongeza umaarufu kwa mashabiki wake kutokana na umahiri
wake wa kushusha mistari ya hip hop mikavu mikavu,kama aonekavyo
jukwaani akiwaimbisha mashabiki wake ndani ya uwanja wa Kambarage usiku
huu.


Baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi
usiku huu kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga,ambapo tamasha la
Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kufanyika.

Mwanadada Linah akiimba sambamba na shabiki wake jukwaani usiku huu
wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa
Kambarage,mkoani Shinyanga usiku.

Baadhi ya Wadau wakubwa na wadhamini wa Tamasha la Serengeti Fiesta
2013,kutoka kampuni ya Serengeti Breweries,Octavian,Bahati pamoja na
mdau wao,wakiwa katika picha ya pozi usiku huu ndani ya uwanja wa
Kambarage,mkoani Shinyanga

Mwanadada ambaye kwa sasa ameonekana akifanya vyema kwenye jukwaa la
Serengeti fiesta 2013,Neylee akiwaimbisha mashaniki wake (hawapo
pichani).

Anajiita Jita Man kutoka jijini Mwanza akitumbuiza jukwaani usiku huu.

Dj Zero kutoka Clouds FM akiburuza mangoma usiku huu.


Mwanadada Shilole na madensa wake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku
huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa
Kambarage.mkoani Shinyanga.


Masbabiki kibao waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta
2013,usiku wakifuatilia na kushangweka vilivyo mbele ya jukwaa la
fiesta.

mashabiki wakifuatilia

Kutoka Wanaume TMK,wakiongozwa Mh Temba na Chege kwa pamoja
wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa
kambarage mjini Shinyanga.

Weusi wakitumbuiza jukwaani usiku huu.

Shabiki akifurahi jamboo.

Kundi la Wanaume TMK-Halisi likiongozwa na Sir Juma Nature
wakilishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa
Kambaraje,mjini Shinyanga.









